SEKRETARIETI ZA MIKOA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA ZATAKIWA KUWASILISHA MPANGO KAZI WA MATUMIZI YA FEDHA 2023/23
Na. Angela Msimbira, OR-TAMISEMI
Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zimitakiwa kuanda taarifa ya mpango kazi wa mtiririko wa Fedha na manunuzi kwa mwaka 2022/23 na kuwasilisha katika Ofisi ya Rais TAMISEMI kabla ya July 20, Mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia TAMISEMI Ramadhani Kailima leo wakati wa kufunga kikao kazi cha makatibu tawala wasaidizi sehemu ya Mipango, Uratibu na Usimamizi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Maafisa Mipango, Takwimu na Ufatiliaji na Waweka Hazina wa Halmashauri leo Jijini Dodoma
Kailima amesema kuwa Mikoa inatakiwa kuhakikisha inakamilisha marekebisho yote ya bajeti ili iweze kuingizwa katika mfumo wa matumizi kabla ya tarehe Julai 11 mwaka huu na kuzitaka Halmashauri zinazopokea fedha za hisani za makampuni kwa jamii zihakikishe fedha hizo zinaingizwa kwenye mipango ya bajeti za Halmashauri husika.
Amesisitiza kuwa Mikoa ifanye uchambuzi wa fedha za maendeleo zinazopelekwa katika miradi ya maendeleo kulingana na asilimia 40 kwa 60 za uchangiaji kutokana na kuhakikisha fedha hizo zinatekeleza miradi ya maendeleo iliyopangwa na Serikali.
“Nendeni mkahakiki maeneo ya utekelezaji wa miradi kabla ya fedha za miradi kutolewa ili kujiridhisha na maeneo hayo kutokuwa na migogoro ya umiliki wa ardhi”, amesisitiza Kailima
Ameendelea kuziagiza Sekretarieti za Mikoa kuhakikisha wanazisimamia Halmashauri kuhakiki maeneo yatakaojengwa miradi ya maendeleo kama elimu na afya kupimwa na kupata hati miliki kisheria.
Aidha amezitaka Sekretarieti za Mikoa kuhakikisha Halmashauri zinaandaa taarifa ya miradi viporo iliyopo katika maeneo yao na kubainisha sababu za kuwepo miradi hiyo na kuwasilisha Ofisi ya Rais -TAMISEMI kabla ya tarehe 25/07/2022
MWISHO
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.