Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wamefanya maandamano ya kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kuwa mgombea urais mwaka 2025 kupitia CCM, pamoja na kumshukuru kwa kumteua Dkt. Emmanuely Nchimbi kuwa mgombea mwenza.
Maandamano hayo yaliandaliwa kuunga mkono maazimio ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM uliofanyika hivi karibuni jijini Dodoma, ambapo wajumbe walimchagua Dkt. Samia kuwa mgombea urais wa Tanzania Bara, Dkt. Nchimbi kuwa mgombea mwenza, na Dkt. Hussein Mwinyi kuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Akizungumza wakati wa kufunga maandamano hayo, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Nyasa, Komredi Clavian Matembo, alisema wamefurahishwa na maamuzi ya chama na wanaunga mkono uteuzi wa Dkt. Samia na Dkt. Nchimbi. Alisema, “Tunaamini maazimio haya ni ya busara, na Umoja wa Vijana wa Nyasa tuko pamoja na chama chetu katika safari hii.”
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tanzania Bara, CDE Mussa Mwakitinya, aliwapongeza vijana wa Nyasa kwa kuandaa maandamano ya amani kama ishara ya kuunga mkono maamuzi ya chama.
Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, amefurahishwa na uteuzi wa Dkt. Samia, akisema kuwa wananchi wa Nyasa wana imani kubwa naye kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo aliyosimamia.
Maandamano hayo yalianzia katika ofisi ya CCM Nyasa, yakapitia maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na barabara ya mzunguko, stendi kuu ya Mbamba Bay, na Baylive, kisha kurudi ofisi kuu ya CCM Nyasa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.