Machifu kutoka ndani na nje ya Tanzania wametembelea eneo la makumbusho lililopo kata ya Maposeni, wilaya ya Songea mkoani Ruvuma , ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kilele cha kumbukizi ya mashujaa wa Vita ya MajiMaji imbacho kitafanyika , tarehe 27 Februari 2025 katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji mjini Songea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Kanali Ahmed Abbas Ahmed, ambaye alikuwa mgeni rasmi, amewapongeza machifu kwa mshikamano wao na ushirikiano mzuri katika kudumisha mila na utamaduni.
, Amemshukuru Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake katika kulinda na kuendeleza utamaduni wa Taifa.
Kanali Abbas pia amewapongeza wakazi wa Maposeni kwa kujitokeza kwa wingi na kuwasihi waendelee kushiriki kwa hamasa siku ya kilele cha kumbukizi ili kuwaenzi mashujaa 67 waliopoteza maisha yao katika vita hivyo mwaka 1906.
Amewataka waandaaji wa kumbukizi hizo kuhakikisha zinaendelea kufanyika kila mwaka ili historia hii muhimu isisahaulike kwa vizazi vijavyo.
Mgeni rasmi katika kilele cha kumbukizi ya mashujaa wa Vita ya MajiMaji anatarajiwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.