HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma wamefanya kikao cha tathimini ya Mkataba wa Lishe cha robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Akitoa taarifa ya mafanikio ya utekelezaji wa mpango wa Lishe kwa kipindi cha robo ya pili Afisa Lishe Jovenary Ndelagi amesema wamefanikiwa kufanya tathimini na kutoa elimu ya lishe na mtindo bora wa maisha kwa vijana rika balehe 365 katika shule tatu za Msingi na shule mbili za Sekondari.
Amesema wamefanikiwa kutoa elimu ya lishe kwa wazee 137 katika maadhimisho ya wiki ya wazee Duniani Oktoba Mosi 2023, katika ,Kata ya Lituta,pamoja na usambazaji wa matone ya vitamini A katika vituo 21 vya kutolea huduma ya afya kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 59.
Ndelagi amesema wamefanikiwa kutoa elimu ya lishe kwa vikundi vya wanawake vitano juu ya ulaji na mtindo bora wa maisha katika vijiji 3 Madaba,Lituta na Kipingo.
“Katika kipindi hicho tumefanikiwa kutoa elimu kwa wanaume 354 juu ya ushiriki wa wanaume katika matunzo ya wanawake wajawazito,wanaonyonyesha na watoto chini ya miaka mitano katika kijiji cha Ngadinda,Ifinga na Mbangamawe”
Hata hivyo ameitaja mikakati waliyojiwekea ili waweze kuboresha na kuifikia jamii kwa uwigo mpana zaidi ikiwa Halmashauri imetenga fedha kupitia mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ili kufanya mafunzo rejea ya kuwajengea uwezo wahudumu wa afya ngazi ya jamii.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile amewaagiza watendaji Kata kutoa elimu katika siku maalumu za lishe kwa kubadilishana Kata ili kutilia mkazo katika Jamii suala la Lishe..
Ndile ameagiza kuboresha lishe kwa watoto kuanzia chekechea hadi Sekondari ambapo amesisitiza elimu ya Kujitegemea ipewe kipaumbele hasa kila shule kuanzisha bustani ya mboga
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.