HALMSHAURI ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma imeweka mikakati 17 ya Kitaaluma Mwaka 2024 ili kuinua ufaulu wa Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi kutoka asilimia 87.62 hadi asilimia 95.
Afisa Elimu Taaluma wa Halmashauri hiyo Rashid Hashim Pilly ameitaja mikakati hiyo katika Kikao cha Tathimini ya Matokeo ya darasa la saba 2023 ambapo Halmashauri ya Madaba imeshika nafasi ya kwanza Kati ya Halmashauri 8 za Mkoa wa Ruvuma.
Pilly amesema Mikakati hiyo ni pamoja na kuwa na Mitihani miwili ya Utamilifu (Mock) Wilaya kwa darasa la saba na mitihani miwili ya upimaji kwa darasa la nne pamoja na kuwepo kwa kalenda moja kiwilaya ya ufanyikaji wa mitihani ya mihula na nusu muhula.
Amesema kutakuwa na Majaribio ya Wilaya kila mwezi kwa darasa la saba ,utafanyika mtihani ngazi ya Kata na Shule,kufundisha kwa muda waziada kabla ya kuanza masomo saa 1 .00 asubuhi na baada ya masomo saa 9.30 hadi 11.00.
Halmashauri ya Madaba ni miongoni mwa Halmashauri tatu zinazounda wilaya ya Songea inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Kapenjama Ndile
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.