• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MADAKTARI bingwa 40 kuanza kutoa huduma hospitali zote za Halmashauri Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: May 5th, 2024

Huduma za mkoba za madaktari Bingwa  zinatarajia kuanza kutolewa katika hospitali za Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma kuanzia  Mei sita hadi 10 mwaka huu.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Louis Chomboko amesema timu ya madaktari bingwa 40  ipo mkoani Ruvuma na inatarajia kuripoti kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed Mei 6 mwaka huu kabla ya Kwenda kuanza kazi ya kutoa huduma katika hospitali za Halmashauri.

Dr.Chomboko amewataja madaktari Bingwa ambao wapo mkoani Ruvuma kwa ajili ya kuanza kutoa huduma za kibingwa ni Pamoja na madaktari wa magonjwa ya wanawake na uzazi,madaktari bingwa wa Watoto na Watoto wachanga,madaktari bingwa wa magonjwa ya ndani,madaktari bingwa wa upasuaji na wabobezi wa mfumo wa mkojo na madaktari bingwa wa usingizi na ganzi.

Amezitaja hospitali ambazo madaktari hao watatoa huduma hizo ni Pamoja na hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo,Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Mbinga,Hospitali ya Halmashauri ya Madaba na Hospitali ya Halmashauri ya Songea iliyopo Mpitimbi.

Hospitali nyingine amezitaja kuwa ni hospitali ya  Wilaya ya Tunduru,hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na kituo cha Afya Mji Mwema kilichopo Manispaa ya Songea.

Natoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kujitokeza katika hospitali hizo kupata huduma za kibingwa ,serikali imewasogezea madaktari bingwa kwenye maeneo yenu hivyo kuwapunguzia gharama za kusafiri umbali mrefu kufuata huduma  za kibingwa,mgonjwa anaweza kutumia bima au fedha taslimu’’,alisema Dr.Chomboko.

Baadhi ya majengo katika hospitali ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma ambayo yatatumika kutoa huduma na madaktari bingwa waliopo mkoani Ruvuma

Baadhi ya majengo katika hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea  iliyojengwa kijiji cha Mpitimbi yatatumika kutoa huduma za kibingwa

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBUNGE Kawawa aleta neema Namtumbo

    May 11, 2025
  • KIONGOZI Mwenge wa uhuru ashiriki upandaji miti Songea

    May 11, 2025
  • MWENGE wa uhuru waweka jiwe la msingi shule ya amali Songea

    May 11, 2025
  • MWENGE wa uhuru wazindua jengo la EMD Peramiho

    May 10, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.