• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MADAKTARI bingwa wa Samia waanza kazi Ruv

Imewekwa kuanzia tarehe: October 29th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema huduma za kibingwa na ubingwa bobezi zinazotolewa na madaktari wa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni muhimu katika jamii kwani zinatoa nafasi kwa wananchi kupata huduma stahiki.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi  wa kambi ya matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi ya Dkt. Samia Suluhu Hassan awamu ya pili uliofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

"Ni ukweli usiopingika huduma hii ni muhimu kwa jamii yetu hasa kwa vituo vinavyotoa huduma katika ngazi ya afya ya msingi, matarajio yangu ni kuwa uwepo wenu katika kambi hii utatoa nafasi kwa wananchi kupata huduma stahiki," alisema Kanali Ahmed.

Ameongeza kuwa wataalam hao wataifanya kazi yao kwa ufanisi mkubwa, kwa kuwa Serikali imeboresha upatikanaji wa vifaa tiba na vituo vya kutolea huduma za afya vinaendelea kuboreshwa ikiwemo ujenzi na ukamilishwaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Hospitali za Halmashauri na Zahanati.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr. Louis Chomboko amebainisha kuwa madaktari hao watatoa huduma za kibingwa za magonjwa ya wanawake  na ukunga, magonjwa ya ndani, magonjwa ya watoto na watoto wachanga, upasuaji na mfumo wa mkojo, mifupa na ajali pamoja na magonjwa ya kinywa na meno.

Dr. Chomboko amelitaja lengo la madaktari hao kufika mikoani ni kusogeza huduma kwa wananchi na kuendeleza dhana ya kupata huduma bora.

Kwa upande wake Dr. Philip Steven Muhonji akizungumza kwa niaba ya madaktari bingwa amesema wao kama wahudumu wa afya wapo tayari kutoa huduma ili kutimiza adhma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

Amesema zoezi hilo linaambatana na kuwajengea uwezo wataalam wengine katika maeneo ambayo bado hayajakamilika kwa kuwa huduma zitakapokuwa zinatolewa ndipo wataalam wengine wanajengewa uwezo.

Awamu ya kwanza ya huduma za kibingwa na ubingwa bobezi za madaktari wa Dkt. Samia Suluhu Hassan zilitolewa kuanzia tarehe 6 hadi 10 Mei mwaka huu, na awamu hii ya pili huduma zinatolewa kuanzia Oktoba 28 hadi Novemba 3 mwaka huu.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.