Kampuni ya Resource Mining Corporation Ltd (ASX:RMI) imegundua uwepo wa madini ya nikeli (nickel) na shaba (copper sulphide) katika Mradi wa Nickel wa Liparamba wilayani Nyasa mkoani Ruvuma nchini Tanzania, hii ikiwa ni uthibitisho wa kwanza wa uwepo wa madini hayo katika eneo hilo.
Kampuni hiyo ambayo imejikita katika uchimbaji wa madini ya kutengenezea betri ilifanya ugunduzi huo mwezi Septemba 2023.
Kampuni hiyo ya Australia pia itafanya mapitio ya matokeo hayo ili kuamua ni programu zipi za uchunguzi zaidi zitakazofanywa ndani ya maeneo ya miradi ya sasa na kwa eneo kubwa zaidi.
Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Asimwe Kabunga ameeleza kuwa kugunduliwa kwa madini hayo ndani ya Mradi wa Nickel wa Liparamba ni matokeo mazuri na yanayoleta fursa ya kusisimua kwa kampuni yao
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.