Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbinga Ndg. Joseph Mdaka amewapongeza madiwani wa Wilaya ya Mbinga kwa kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali katika maeneo yao.
Pongezi hizo zimetolewa katika maadhimisho ya miaka 47 ya chama cha mapinduzi yaliyofanyika Kiwilaya katika Kata ya Maguu Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
“ Niwapongeze sana madiwani wote wa Wilaya ya Mbinga mnafanya kazi kubwa na inaonekana, endeleni kushirikiana na wataalam katika kuwaletea wananchi maendeleo” Amebainisha Mdaka
Aidha Mdaka amewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto shule ili waweze kupata elimu, amebainisha kuwa Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya elimu ili boresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo amewataka wananchi wa Wilaya ya Mbinga kuhakikisha wanaimarisha amani katika maeneo yao hasa katika kipindi tarajiwa cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“ Amani ni msingi wa kuleta maendeleo katika nchi yetu sehemu yoyote isiyo na amani haina maendeleo, tuilinde amani yetu”Amesisitiza Mangosongo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.