Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa limepongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw. Khalid Khalif Kwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Pongezi hizo zimetolewa katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya pili ambacho kililenga kujadili taarifa za mbalimbali za maendeleo ya Halmashauri hiyo ambapo kilifanyika kwenye ukumbu wa Ofisi ya Mkurugenzi Wilaya ya Nyasa
Akiongea kwa niaba ya Baraza la Madiwani Mwenyekiti wa Halmshuari ya Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Sterwat Nombo amempongeza Mkurugenzi huyo Kwa ukusanyaji Bora wa mapato ya Ndani ambao umefikia asilimia 112 ya makusanyo kwa bajeti y amwaka 2023/2024.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.