Baraza la madiwani Halmashauri ya wilaya songea wamefanya kikao cha kupokea taarifa ya hesabu za Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha ulioishia 30, juni 2022
Kikoa hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Songea Mhe, Menasi Komba ambapo kimeudhuriwa na mkuu wa wilaya hiyo Mhe, Pololet Mgema, watumishi pamoja na madiwani.
Taarifa ya hesabu za Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa mwaka wa Fedha ulioishia 30, juni 2022 inaonesha Halmashauri imevuka malengo ya ukanyaji mapato kwa kukusanya jumla ya Zaidi ya asilimia 123 na kushika nafasi ya tano kitaifa kiukusanyaji mapato.
Naye Muhasibu wa Halmashauri mwandamizi Viviano Ndunguru akiwasilisha na kuisoma taarifa hiyo ya mbele ya baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo amesema kuwa kwa mujibu wa Sheria ya fedha ya Serikali za mitaa Halmashauri zote nchini zinatakiwa kufunga hesabu na kuwasilisha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za seikali (CAG)
“kazi ya ufungaji wa hesabu kwa mwaka 2021/2022 ilianza tarehe 10 july na imekamilika tarehe 25 sept 2022 taarifa hii inaonyesha taarifa ya mapato na matumizi katika Halmashauri, taarifa zimetolewa katika mfumo wa muse kama muongozo wa ufungaji hesabu ambao ni mfumo utumikao serikalini” alisema Viviano.
Naye Filbert Mendrad Soko ambaye Diwani wa Kata ya Liganga iliyopo halmashauri ya Songea, amesema kuwa taarifa hiyo wao kama madiwani wameipokea vizuri hivyo matarajio yao ni kuendelee Zaidi kufanya vizuri katika ukusanyaji mapato katika mwaka wa fedha ujao.
“Matarajio yetu sasa kwa mwaka huu wa fedha 22/23 kukusanya fedha Zaidi ya mapato ya ndani kwasababu bajeti yetu ya ndani imevuka na kuangalia mianya yote inayotorosha mapato kuweza kidhibiti ili kuweza kufikia lengo itakapofikia juni 2023”alisema Soko.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.