• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MADIWANI Songea wacharuka Halmashauri kushika mkia

Imewekwa kuanzia tarehe: February 13th, 2021

BARAZA la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Songea limesikitishwa na  wasimamizi wa Idara ya Elimu kushindwa kusimamia taaluma na kusababisha Halmashauri hiyo kushika mkia kati ya Halmashauri nane za Mkoa wa Ruvuma kwenye matokeo ya darasa la saba 2020.

Matokeo ya mtihani wa Taifa wa Darasa la saba 2020,yanaonesha kuwa Halmashauri hiyo ilifaulisha kwa asilimia 66.66 hivyo kuwa ya mwisho kimkoa.

Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la madiwani,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Menas Komba ameiagiza  Idara ya elimu msingi na sekondari kuanza kuchukua hatua kwa wasimamizi na walimu ambao hawafanyikazi.

“Sisi kama Baraza la madiwani sasa tutashughulika nao,tunataka Halmashauri ya Songea kielimu tuwe juu,serikali imetoa fedha za utoaji wa elimu bure,waratibu elimu kata wamepewa pikipiki,wanalipwa posho za madaraka shilingi 250,000 kila mwezi,wakuu wa shule za msingi wote wanalipwa posho za madaraka hawafanyi kazi kikamilifu’’,alisisitiza Komba.

Ametoa rai kwa maafisa elimu na wanaohusika kuchukua hatua na kwamba wanaoshindwa kusimamia elimu  ameshauri wasihamishwe badala yake washushwe vyeo na kwa kutoa mapendekezo kwa Mkurugenzi na kuletwa kwenye kikao cha madiwani ili kushughulika nao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu,Afya na Maji katika Baraza hilo Manfred Mzuyu amesema kamati yake ilifanya utafiti kwa kutembelea kata,baada ya matokeo mabaya ya elimu ya msingi na kubaini kuwa  baadhi ya waratibu elimu kata, pikipiki walizopewa na serikali wanazitumia kwa matumizi yao na hawaishi kwenye vituo vyao vya kazi.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kizuka Jacob Nditi amesema,uchunguzi walioufanya wamebaini wasimamizi wa elimu wakiwemo waratibu Elimu Kata na walimu wakuu baadhi yao hawasimami walimu ili kujua iwapo walimu wanafundisha ipasavyo.

“Kwanini  baadhi ya waratibu hawaishi kwenye vituo vyao vya kazi,sababu ni nini zinazosababisha  kupata ufaulu wa chini sana na kusababisha Halmashauri yetu kupata aibu’’,alihoji Diwani  Nditi.

Naye Diwani wa Kata ya Mpitimbi Issa Said Kindamba amesema iwapo walimu wangewajibika ipasavyo darasani kwa usimamizi wa walimu wakuu,Halmashauri isingepata  ufaulu wa hatari na kusababisha Halmashauri kushika nafasi  ya mwisho kimkoa.

“Wilaya yetu imechafuka kwa sababu ya kutofahamu mtu na uwajibikaji wake kwenye eneo ambalo anasimamia,naomba utengenezwe mfumo wa  walimu kutambua wajibu wao kwa watoto na Taifa’’,alisema.

Diwani wa Kata ya Kilagano ametoa rai kwa timu ya ukaguzi wa elimu,kueleza changamoto zipi zinazoikabili sekta ya elimu hadi kutoa matokeo ya chini ya ufaulu.

Akijibu hoja hizo Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Songea Tanu Kameka amekiri ufaulu sio wa kuridhisha ambapo ameyataja matokeo ya mwaka 2019 ya darasa la saba Halmashauri ilifaulisha kwa asilimia 71.99 na mwaka 2020 ufaulu ulikuwa wa asilimia 66.66.

Kameka amesema wamefanya tathmini  ya elimu kwa kupita kata zote na kuwahusisha wadau wote wa elimu ambapo hivi sasa wanakusudia kufanya ufuatiliaji wa hali ya juu mwaka mzima na kuchukua hatua kwa wasimamizi wa elimu.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Februari 13,2021

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.