Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma Mhe. Peres Magiri, amewataka wananchi wa wilaya hiyo kujiandaa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo yanayotarajiwa kutokea muda mfupi ujao.
Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nyasa, Mhe. Magiri alieleza kuwa wilaya hiyo inakwenda kufungua fursa nyingi za maendeleo.
Amezitaja fursa hizo kuwa ni pamoja na ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay, ambayo ikikamilika, itakuwa kitovu cha biashara. Wafanyabiashara wakubwa waliokuwa wakifanya biashara Kariakoo, Dar es Salaam, wanatarajiwa kufungua maduka Nyasa na kufanya biashara na wananchi wa Tanzania, Malawi, na Msumbiji.
Aidha, alieleza kuwa wilaya hiyo ina vivutio vingi vya utalii kama Ziwa Nyasa, Fukwe za Ziwa Nyasa, Mlima Mbamba, na visiwa vya Mbamba Bay na Lundo, hivyo wananchi wanapaswa kujiandaa ili kunufaika na fursa hizo.
Mhe. Magiri amewahimiza wananchi na watumishi wa serikali kuweka mikakati ya kunufaika na uwekezaji, hususan katika ujenzi wa hoteli, nyumba za kulala wageni, na maeneo mengine ya biashara.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.