• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MAFUNZO ya uhifadhi yafungwa Namtumbo wahifadhi 97 wa TANAPA wafuzu

Imewekwa kuanzia tarehe: October 1st, 2022

ASKARI UHIFADHI WA TANAPA 97 WAHITIMU MAFUNZO NAMTUMBO

ASKARI wahifadhi  wa TANAPA 97 wamehitimu mafunzo  ya aina tatu tofauti katika chuo cha Uhifadhi Maliasili Jamii cha Likuyu Sekamaganga wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.

Akitoa taarifa ya mafunzo hayo kwenye hafla ya ufungaji mafunzo hayo iliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho,Naibu Kamishina wa Uhifadhi  na Mkuu wa  Kanda wa Kusini Asteria Ndaga alisema kati ya wahitimu,askari Uhifadhi 52 wamehitimu mafunzo ya awali ya ajira mpya. 

Kamishina Ndaga amewataja maafisa Uhifadhi saba na Askari  Uhifadhi mmoja wamehitimu mafunzo ya mabadiliko ya utendaji kazi kutoka mfumo wa kiraia na Kwenda kwenye mfumo wa kijeshi na  maafisa Uhifadhi Daraja la pili wapatao 37 wamehitimu mafunzo ya awali ya Uongozi.

Hata hivyo Ndaga amesema mafunzo hayo yalifunguliwa katika vipindi vitatu tofauti yakijumuisha wanawake saba na wanaume 90 ambapo kati yao 44 ni maafisa uhifadhi na  53 ni Askari Uhifadhi na kwamba mafunzo yalifundishwa kwa njia ya nadharia na vitendo.

Amezitaja mada mbalimbali zilizofundishwa kuwa ni  uzalendo,maadili, kuzuia na kupambana na rushwa,elimu ya uhifadhi na utalii,uraia,uchunguzi,utoaji Ushahidi mahakamani,namna ya kuandaa hati za mashitaka,sheria za ulinzi,utunzaji wa vielelezo, mafunzo ya uongozi na mifumo mbalimbali inayotumika katika uhifadhi.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika ufungaji wa mafunzo hayo Naibu Kamishina wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara Herman Batiho  amewapongeza wahitimu wote kwa kuhitimu mafunzo hayo muhimu ambayo amesema yamewajengea uwezo wa usimamizi wa rasilimali za wanyamapori na misitu ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa.

“Ni matumaini yangu mafunzo haya yamewajengea uzalendo,uadilifu,ujasiri,utayari,kujiamini Pamoja na kuwapa mbinu na ari kubwa katika kulinda maliasili za Taifa’’,alisisitiza Kamishina Batiho.

Hata hivyo aliwataka wahitimu kuhakikisha  mafunzo hayo wanayafanya kwa vitendo katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku kwenye vituo vyao vya kazi na kusisitiza kuwa mbinu walizojifunza kwenye mafunzo hayo zikawe chachu katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za uhifadhi hususan kukabiliana na majangili.

Naye Kamishina Msaidizi Mwandamizi na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere Witness Shoo amewaasa wahitimu kuhakikisha wanafanya kazi kwa uaminifu kwa sababu serikali tayari imewapa ajira ambayo ni dhamana kwao.

Mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo Afisa Uhifadhi TANAPA Mwandamizi Ombeni Gingi akizungumza kwa niaba ya wenzake ameahidi kutumia mafunzo hayo katika kusimamia rasilimali za Taifa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Chuo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii Likuyu Sekamaganga Namtumbo kilianzishwa mwaka 1995 kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Shirikisho la Ujerumani.

Imeandikwa na Albano Midelo

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ruvuma

Oktoba Mosi,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBUNGE Kawawa aleta neema Namtumbo

    May 11, 2025
  • KIONGOZI Mwenge wa uhuru ashiriki upandaji miti Songea

    May 11, 2025
  • MWENGE wa uhuru waweka jiwe la msingi shule ya amali Songea

    May 11, 2025
  • MWENGE wa uhuru wazindua jengo la EMD Peramiho

    May 10, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.