MAFUNZO ya Sensa ngazi ya Wilaya kwa awamu ya tatu yameanza rasmi Mkoani Ruvuma kwa Makarani na wasimamizi wa Maudhui.
Hayo ameyasema Mratibu wa Sensa wa Mkoa wa Ruvuma Mwantumu Athumani baada ya kutembelea katika Halmashauri ya Songea na Manispaa ya Songea .
“Mafunzo Ngazi ya tatu yameanza na yatafanyika kwa siku 19 kila siku bila kupumzika na kuhusisha nadharia na vitendo”.
Mratibu amesema mafunzo hayo yamejumuisha na watendaji kata kwa siku mbili ili wakahakikishe wanafanya uhamasishaji kwa wananchi.
Hata hivyo ametoa rai kwa wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma wawe tayari kuhesabiwa ikiwemo kupata taarifa za watu watakaolala kwenye kaya ikiwa ni pamoja na wageni wahesabiwe mara moja tu.
Aidha mratibu amesema wananchi wahakikishe wanaweka vitamburisho vya Taifa, vya kupigia kura pamoja na vya ujasiliamali viandaliwe ikiwa moja ya karani afikapo kuchukua taarifa aweze kuchukua taarifa kwa urahisi.
Kwa Upande wake Mtendaji kata ya Fedeferm Manispaa ya Songea Afidhi Bakariamesema zoezi la Sensa na watu na Makazi kwa mara ya kwanza linafanyika kwa mfumo wa kidigitali hivyo Serikali imewekeza fedha nyingi.
Bakari ametoa rai kwa Watendaji Kata wote Nchini washiriki mafunzo na watambue kinachoenda kufanyika katika Kata na Mitaa yote.
“Watendaji wenzangu tuhakikishe watu wote katika Kata na Mitaa wanahesabiwa itakuwa si busara watu wakashindwa kuhesabaiwa kwa sababu Serikali imewekeza Fedha nyingi”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Julai 31,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.