• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Songea yazindua wiki ya sheria

Imewekwa kuanzia tarehe: January 27th, 2025

Mkuu  wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, amesema Mahakama ndio chombo pekee chenye wajibu wa kupiga vita dhuluma, uonevu, ukwepaji kodi, ubadhilifu wa mali za umma na matumizi mabaya ya mamlaka.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini kwa Kanda ya Songea uliofanyika katika viwanja vya soko kuu la Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

"Ni dhahiri kuwa Mahakama ina kazi ya kupiga vita dhuluma, uonevu, ukwepaji kodi, ubadhilifu wa mali za umma, matumizi mabaya ya mamlaka au ofisi, kwa kuwa mahakama ndio chombo pekee chenye wajibu huo, nawaomba mfanye kazi zenu bila urasimu ama ukiritimba, na katika kufanya hivyo sio tu kwamba mtazidi kuheshimika bali pia mtapata thawabu mbele za Mwenyezi Mungu," alisema Kanali Ahmed.

Amewakumbusha wananchi kuwa chombo pekee cha kutatua mgogoro au shauri la aina yoyote ni Mahakama na sio sehemu nyingine, isipokuwa kwenye migogoro ambayo sheria imezipa taasisi zingine mamlaka ya kuisikiliza ili kuondoa migongano ya kimaslahi kati ya Mahakama na taasisi zingine.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha, amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka 2025 inayosema "TANZANIA YA 2050; Nafasi ya taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya dira ya taifa ya maendeleo" imebeba ujumbe mzito juu ya wajibu wa Mahakama na taasisi zinazoshughulikia haki madai katika kuhakikisha wanafikia malengo ya Dira ya mpango wa maendeleo ya Tanzania ya Mwaka 2050.

Amesema katika wiki hiyo ya sheria, Mahakama pamoja na wadau wa sheria watawaelimisha wananchi ndani ya mkoa wa Ruvuma juu ya shughuli za Mahakama kama chombo chenye mamlaka ya utoaji haki kikatiba na jinsi wadau na wananchi wanavyoshirikiana na chombo hicho katika utoaji haki, umuhimu wa amani, uzingatiaji wa sheria, kukwepa matumizi ya nguvu na kuchukua sheria mkononi ili kujenga misingi imara ya amani, mshikamano na umoja kwenye mkoa.

Ameongeza kuwa wananchi wataelimishwa kuhusu maboresho yanayoendelea ndani ya mahakama ikiwa ni pamoja na matumizi ya TEHAMA, ambapo watapewa elimu na wataalamu namna ya kupakua hukumu yake moja kwa moja kutoka mtandao unaoitwa TanzLII badala ya kusubiri hukumu iliyosomwa katika jengo la Mahakama Kuu, hivyo wananchi watumie wiki ya sheria kupata na kuongeza maarifa ya kisheria.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.