Serikali ya Tanzania imendelea kuboresha huduma za afya kwa kuongeza idadi ya hospitali zenye majengo ya kutolea huduma za dharura (EMD) kutoka 7 hadi kufikia 116 ndani ya miaka minne ikiwa ni ongezeko la hospitali 109.
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema hayo wakati akifunga maadhimisho ya juma la afya kitaifa pamoja na kuzindua mfuko maalum wa ufadhili wa masomo kwa Madaktari Bingwa na Bobezi kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Waziri Mhagama amesema kukamilika kwa ujenzi wa majengo ya kutolea huduma za dharura kunapunguza vifo na kuokoa maisha kwa wagonjwa wa dharura na wa ajali.
Kuhusu huduma ya magari ya wagonjwa Waziri Mhagama amesema idadi ya magari ya imeongezeka kutoka 540 mwaka 2020 hadi 1,267 jambo linalorahisisha huduma za dharurana kuwafikia wananchi wenye changamoto za afya.
“Magari haya yanakwenda kusaidia kusafirisha watu wenye changamoto za afya wakiwemo akinamama wenye changamoto za uzazi kwa haraka na kuwafikisha katika huduma za rufaa na hivyo kupunguza adha kwa wananchi na kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika,” amesema Mhe. Mhagama.
Aidha, Waziri Mhagama amezishukuru Sekta binafsi nchini kwa kuunga mkono Serikali katika kutoa huduma bora kwa wananchi kuanzia ngazi ya msingi hadi ya Kitaifa.
“Kazi hii mnayoifanya kwa kushirikiana na serikali inatupeleka mahali pazuri kwa kuimarisha huduma za kinga kwa magonjwa, matumizi ya teknolojia zitakazotupelekea kutoa huduma stahiki kwa jamii,” amesema.
Naye Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema wanaposheherekea Siku ya Afya Duniani huku Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amepokea tuzo ya Global Gates Keepers Award inaonyesha taswira ya maendeleo makubwa katika sekta ya Afya akiwa ni miongoni mwa marais saba waliopokea tuzo hiyo ambapo ameielekeza kwa watumishi wa afya ikiwa ni kuthamini mchango wao katika kutoa huduma.
Akitoa salam za Ofisi ya Rais - TAMISEMI Naibu Waziri anayeshughulikia Afya , Dkt. Festo Dugange amesema Sekta ya Afya imeendele kuboresha mshikamano wa sekta hiyo ili kuhakikisha mwananchi wanaowahudumiwa na wanapata huduma bora za afya popote alipo nchini.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.