Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema serikali itaendelea kuboresha maslahi ya wahudumu wa afya kwa kuhakikisha inaboresha Maisha yao na vitendea kazi.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizindua Jengo la Mionzi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma katika Kata ya Mwengemshindo Manispaa ya Songea,akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo. Ametoa wito kwa watoa huduma za afya kutunza vifaa tiba ikiwemo kuweka utaratibu mzuri wa matengenezo ili viweze kutoa huduma kwa wananchi wakati wote.
Makamu wa Rais amesema ni dhamira ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha inasogeza huduma bora za afya karibu na wananchi ikiwemo kupeleka vifaa tiba vya kisasa katika hospitali za mikoa ili kuwapunguzia gharama wananchi kufuata huduma hiyo maeneo ya mbali.
Aidha Makamu wa Rais amesema Serikali inathamini mchango wa watoa huduma za afya kwa kuwa wanamchango mkubwa katika kuwahudumia wananchi na kuokoa Maisha yao. Amewasihi wahudumu wa afya kuendelea kuwahudumia wananchi kwa upendo mkubwa.
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango anaendelea na ziara ya kikazi mkoani Ruvuma yenye lengo la Kusikiliza changamoto za wananchi, kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzindua miradi ya maendeleo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.