Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani ambayo yanafanyika katika uwanja wa Majimaji Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed wakati anatoa taarifa ya maadhimisho hayo kwa wanahabari ofisini kwake mjini Songea.
“Kwa mwaka 2024 maadhimisho hayo yataanza Novemba 21 hadi Desemba Mosi 2024 ambayo itakuwa ni kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI kitaifa mkoani Ruvuma’’,alisema.
Amebainisha kuwa katika maadhimisho hayo,shughuli mbalimbali za afya na kijamii zitatolewa katika uwanja wa Majimaji na nje ya uwanja kwenye Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma katika wiki yote ya maadhimisho.
Kaulimbiu ya maadhimisho kwa mwaka huu inasema chagua njia sahihi,tokomeza UKIMWI ambapo Mkuu wa Mkoa ameitaja kaulimbiu hiyo inakumbusha ;kuzingatia njia sahihi za kitaalamu katika kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI ili kuweza kutokomeza janga la UKIMIWI ifikapo mwaka 2030.
Kanali Abbas ameyataja malengo mahusisi ya maadhimisho hayo kuwa ni kutoa fursa ya kutathmini hali halisi ya mwelekeo wa kudhibiti Virusi vya UKIMWI kitaifa na kimataifa,kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu udhibiti wa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
Malengo mengine ameyataja kuwa ni kuendelea kuhimiza huduma stahiki kwa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU na kuwakumbuka wale wote waliopoteza Maisha kutokana na UKIMWI na kuendelea kufanya uraghabishi kwa viongozi wa serikali na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha ajenda ya UKIMWI inaendelea kuwa vipaumbele vya Mkoa na serikali .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.