Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kupitia Baraza la Madiwani wameweka mikakati madhubuti ya kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa lengo la kuongeza mapato kutoka shilingi bilioni sita hadi bilioni 15 kupitia vyanzo vyake mbalimbali vya Halmashauri hiyo.
Katika kutekeleza mikakati hiyo Madiwani, viongozi wa CCM Mkoa na Wilaya, pamoja na wataalamu wamefanya ziara ya kutembelea Halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani na Halmashauri ya Tanga Jiji mkoani Tanga kwa lengo la kwenda kujifunza namna ya uendeshaji wa miradi ya kimkakati na ukusanyaji wa mapato ya madini ya ujenzi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.