Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Joseph Kashushura amebainisha kuwa mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga yameongezeka kutoka zaidi ya shilingi bilioni 2.65 kwa mwaka wa fedha 2015/2016 hadi kufikia zaidi ya shilingi bilioni 7.584. kwa mwaka wa fedha 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 186
Kashushura alikuwa anatoa taarifa ya mafanikio katika kutekeleza Dira ya Taifa ya maendeleo 2025 na maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 kwenye kikao cha dharura cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya mjini Mbinga
Hata hivyo amesema kupitia mapato hayo na fedha kutoka Serikali Kuu Halmashauri imeweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya Elimu, Afya, Kilimo, Mifugo,Uvuvi na uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.