Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso amepiga marufuku kwa Mamlaka zote za maji nchini kuacha tabia ya kutoa huduma za maji saa nane za usiku.
“Unatoa maji saa nane za usiku afanye nini mwananchi,Katibu Mkuu upo hapa waambie kabisa watendaji wako,huduma ya maji itolewe muda ambao mwananchi anaweza kupata ile huduma bila usumbufu wa aina yoyote’’, alisisiza Waziri wa Maji.
Hata hivyo amesema iwapo kuna hitilafu ya kusababisha huduma ya maji kutopatikana ni vema wananchi wafahamishwe mapema,ambapo amekemea tabia ya kukata maji siku nzima bila kutoa taarifa kwa wananchi hivyo kutengeneza manung’uniko yasiyokuwa ya lazima kwa wananchi.
Amekiagiza Kitengo cha Mawasiliano kwenye Mamlaka za maji kutoa taarifa kwa wakati kwa wananchi ili wafahamu mapema na kujipanga namna ya kuhifadhi maji
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.