KATIBU Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Steven Ndaki amezindua kamati ya Uratibu ya msaada wa kisheria ya Mkoa wa Ruvuma.
Akizungumza katika kikao cha uzinduzi wa kamati hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa amesema Serikali kupitia Wizara ya katiba na Sheria imepewa mamlaka kwa mujibu wa Sheria ya Msaada kwa kisheria na.1 ya 2017.
Ndaki amesema Wizara kupitia ofisi ya Rais Tamisemi imeweza kutoa mafunzo kwa maafisa Maendeleo ya jamii wa Mkoa na Wilaya ambao kwa sasa wanatambulika kama wasajili wasaidizi wa mtoa huduma ya msaada wa kisheria.
Hata hivyo Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa wadau wa msaada wa kisheria kwa ngazi ya Mkoa na jukumu lake kubwa ni kusimamia utekelezaji wa sheria ya msaada wa kisheria na kanuni zake.
“Naomba nisisitize kufanya kazi kwa ushirikiano miongoni mwa wadau kwa lengo la kumsaidia mwananchi wa chini kabisa ambae amekosa uwezo wa kuendesha kesi”.amesisitiza Ndaki
Ndaki amesema vyombo vya habari vitumike katika kutoa elimu ya msaada wa kisheria kwani ni kiungo muhimu katika kufikisha taarifa kwa wananchi.
Kwa upande wake Naomi Ngago Katibu wa chama cha Mawakili Mkoa wa Ruvuma amesema wameendelea kutoa Elimu ya msaada wa kisheria kwa wananchi kupitia redia.
Ngago amesema chama cha Mawakili Ruvuma wamesikiliza mashauri kwenye makosa ya jinai na kushirikiana na Mahakama kuu kutoa mawakili kusimamia kesi zao bure na kuwatembelea magereza na kujua changamoto zao na kuzitatua.
“Tunakuna na changamoto nyingi ikiwemo uwepo wa kesi nyingi lakini bado wanachini hawana elimu ya msaada wa kisheria hawajui pakuanzia hususani watu wa vijijini ,wateja wengi kuomba msaada wakati mda umepita wa kesi zao mara baada ya kwenda kwa mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa ”.
Wakili wa Wizara ya Katiba na Sheria George Molel akitoa mafunzo kwa wanakamati hao amesema msaada wa kisheria hufanywa na mawakili kwenda mahakamani upo katika makosa ya jinai na madai.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Septemba 28,2021.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.