• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MASHINDANO ya UMITAMSHUMTA na UMISETA yazinduliwa rasmi Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: May 29th, 2025

Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA kwa shule za msingi na sekondari katika Mkoa wa Ruvuma yamezinduliwa rasmi  Mei 29 kwenye Uwanja wa Majimaji Manispaa ya Songea, yakishirikisha Halmashauri zote nane za mkoa  wa Ruvuma.

Shughuli hiyo ya uzinduzi ilihudhuriwa na maelfu ya wanafunzi, walimu na viongozi wa serikali.

Akizungumza katika uzinduzi huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Mary Makondo, amesema mashindano ya mwaka huu yanaendeshwa kwa kaulimbiu isemayo: “Viongozi bora ni msingi wa maendeleo ya taaluma, sanaa na michezo. Shiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu.

Kauli hiyo inalenga kuhamasisha vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za michezo pamoja na kuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya taifa kupitia uongozi bora.

Makondo ameongeza kuwa serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejidhatiti kukuza vipaji vya vijana kupitia sekta ya elimu.

Amesema tayari shule za sekondari za Maposeni,Chandarua na Mahanje mkoani Ruvuma zimeanza mchakato wa kuboresha viwanja vya michezo kwa kuweka miundombinu sahihi, hatua ambayo inalenga kuinua kiwango cha mashindano na maandalizi ya wanamichezo kwa ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Katika kuhakikisha mashindano hayo yanazidi kuwa ya ushindani na tija, Makondo amezitaka Halmashauri zote kuweka bajeti maalum ya sekta ya michezo. “

“Michezo ni ajira, ni afya, na ni msingi wa kuibua viongozi wa kesho,” amesema Makondo huku akisisitiza umuhimu wa kuwekeza katika vipaji vya vijana kama njia mojawapo ya kujenga jamii bora yenye nguvu kazi imara.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma, Anthony Luoga , amesema mashindano hayo ya siku nne yamepata mafanikio makubwa kwa kujumuisha jumla ya washiriki 688, walimu 73 na viongozi 27 kutoka halmashauri mbalimbali.

Amesema kupitia mashindano haya, mkoa unatarajia kupata wawakilishi mahiri watakaoshiriki mashindano ya kitaifa yatakayofanyika mkoani Iringa hivi karibuni.

Ameongeza kuwa mwaka huu Mkoa wa Ruvuma unalenga kuunda timu bora itakayoshiriki mashindano ya kimataifa nchini Kenya.

“Tunaamini vipaji vilivyopo Ruvuma vina uwezo wa kupeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa,” amesema kwa msisitizo. .

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.