• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MASHINDANO ya UMITAMSHUMTA na UMSSETA yazinduliwa kwa kishindo Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: May 30th, 2025

Katika uwanja wa Majimaji uliopo mjini Songea, shamrashamra na vifijo vilitawala wakati Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, alipouzindua rasmi msimu wa mashindano ya michezo ya shule za msingi (UMITASHUMTA) na sekondari (UMISSETA) kwa mwaka 2025. 

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, Bi. Makondo aliwataka wananchi na wanafunzi kushiriki mashindano haya kwa amani na mshikamano, sambamba na kaulimbiu ya mwaka huu isemayo: "Viongozi bora ni msingi wa maendeleo ya taaluma, sanaa na michezo, shiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu."

Akielezea hatua madhubuti zilizochukuliwa na serikali kuimarisha sekta ya michezo, Bi. Makondo alisema kuwa shule tatu za Mkoa wa Ruvuma  ambazo ni Maposeni, Chandarua na Mahanje  zimeanza kuboreshwa viwanja vyake kwa kuweka vipimo sahihi vinavyokidhi viwango vya kitaifa. Alibainisha kuwa hatua hii si tu inalenga kuinua kiwango cha mashindano, bali pia inatoa fursa kwa vijana wenye vipaji kuibukia katika jukwaa la kitaifa na kimataifa kupitia maandalizi bora.

Aidha, Bi. Makondo alisisitiza kuwa serikali ya awamu ya sita imedhamiria kukuza michezo, sanaa na utamaduni kwa vitendo. Ameeleza kuwa mbali na kuboresha miundombinu ya michezo, serikali imeongeza idadi ya taasisi zitakazosaidia kukuza vipaji kupitia mitaala ya elimu ya sasa. Hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa michezo si tu burudani bali pia nyenzo muhimu ya kujenga afya, nidhamu na ajira kwa vijana.

Katika kutambua mchango wa Mkoa wa Ruvuma katika maendeleo ya michezo nchini, Bi. Makondo alipongeza serikali kwa kutenga jumla ya shule 56 kwa ajili ya ukuzaji wa michezo, ambapo Mkoa wa Ruvuma umefaidika kwa kupata shule tatu. Hii ni ishara ya wazi kuwa Mkoa huu una nafasi muhimu katika mchango wa kitaifa kwenye sekta ya michezo na maendeleo ya vipaji.

Kwa upande wake, Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma, Anthony Luoga, alifichua kuwa msimu huu Mkoa unajivunia jumla ya wanamichezo 688, walimu 73 na viongozi 27 ambao watauwakilisha mkoa katika mashindano ya kitaifa yatakayofanyika mkoani Iringa. Luoga alieleza kuwa maandalizi ya washiriki hao yamekamilika na matumaini ni makubwa kuwa Ruvuma itang'ara na kurejea na ushindi mkubwa kutoka Iringa.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.