MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema amezindua mahindazo ya Michezo ya umitashumta.
Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya Matogoro Manispaa ya Songea ikijumuisha Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma na kujumuisha Shule za Sekondari na Msingi.
Akizungumza katika halfa hiyo ya uzinduzi Mgema ametoa rai kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kuwezesha Mashindano hayo ili waweze kufanya vizuri na kuchukua ushindi .
“Niwasisitize tunahitaji timu bora itakayo wakilisha Mkoa wetu na tunahitaji wanamichezo sahihi “.
Mgema amesma halmashauri zote zihakikishe zinatoa wanamichezo kwa idadi iliyopangwa kwenye kambi ya Mkoa na kuwezesha shughuli zote zitakazofanyika ili Ruvuma iweze kuwa kinara katika Michezo .
Kwa upande wake Katibu tawala msaidizi upande wa Elimu Emanuel kisongo amesema Mkoa tumeweka maandalizi ya kutosha na ni muhumu sana kushiriki mashindano hayo.
Kisongo ameipongeza Halmashauri ya Madaba kwa kuwa na ushirikiano na Mkoa na kuhakikisha Shule hiyo inakuwa na vigezo vya kutosha kwa kutoa eneo la hekari 50 na Shule hiyo kuwa na sifa .
Vile vile mashindano hayo ya umitashumta kwa mwaka huu 2022 kilele chake kitaifa yatafanyika Mkoa wa Tabora ya kuhusisha Mikoa yote hapa nchini.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.