• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MASOKO ya madini Ruvuma yaingiza bilioni 5.5

Imewekwa kuanzia tarehe: August 3rd, 2020

Masoko ya madini ya vito na dhahabu mkoani Ruvuma tangu kufunguliwa kwake Mei 2019 hadi kufikia Mei 2020 yamenunuliwa madini yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 5.5.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema katika kipindi hicho masoko hayo yaliopo Tunduru na Songea yamewezesha kununuliwa madini yenye uzito wa gramu 390,936.27.

“Mrabaha uliopatikana katika mauzo hayo ni shilingi milioni 332,093,674.35,ada ya ukaguzi iliyopatikana ni shilingi milioni 55,348,945.72 na kodi ya huduma iliyopatikana katika kipindi hicho ni shilingi milioni 16,604,683.72’’,alisema Mndeme.

Mndeme amesema serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli imeendelea na utekelezaji wa shughuli mbalimbali kwa ajili ya kukuza Sekta ya Madini katika Mkoa wa Ruvuma.

Amesema sekta ya Madini Mkoa wa Ruvuma imekuwa kwa kasi katika maeneo ya uwekezaji kwenye leseni za uchimbaji, uzalishaji madini, ajira pamoja na makusanyo ya maduhuli ya Serikali.

Kwa upande wake Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Jumanne Mohamed Nkana  amezitaja Faida za uanzishwaji wa masoko ya madini nchini kuwa ni wachimbaji wa madini kupata bei nzuri ya madini kutokana na uwazi uliopo sokoni.

Faida nyingine amezitaja kuwa ni wachimbaji wa madini kutokuwa na haja ya kutorosha madini, kitendo ambacho kilikuwa ni hatari kwani kilikuwa kinasababisha wachimbaji kupokonywa madini yao na serikali pamoja na kukabiliwa na kifungo pindi wanapobainika kutenda kosa hilo.

Kwa mujibu wa Afisa Madini Mkazi huyo,faida nyingine ni Serikali  kupata takwimu sahihi za mauzo ya mazini na urahisi wa kukusanya mapato yaliyokuwa yakipotea kutokana na utoroshaji wa madini.

“Kuongezeka kwa tija ya utendaji kazi kwenye ofisi za madini kutokana na watumishi wa ofisi hizo kufanya shughuli nyingine badala ya kupoteza muda mwingi kuwafuatilia wachimbaji wa madini migodini,Serikali kupata takwimu sahihi za uzalishaji na mauzo ya madini nchini na Kuongezeka kwa mapato ya serikali yatokanayo na shughuli za uchimbaji na biashara ya madini ni faida nyingine za uwepo wa masoko haya’’,alisisitiza Nkana.

Hata hivyo Katika kutatua changamoto wanazokabiliana nazo wachimbaji wadogo wa Madini mkoani Ruvuma, Serikali inajenga kituo cha Umahiri kwa ajili ya wachimbaji wadogo.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amezitaja faida za kituo hicho kuwa ni uwepo wa takwimu za wachimbaji wadogo katika mkoa wa Ruvuma,upatikanaji wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo na utoaji wa mafunzo na maarifa kwa Wachimbaji wadogo kupitia wadau mbalimbali.

Faida nyingine za kituo hicho amezitaja kuwa ni kuwepo kwa Mfumo wa kutathmini mashapo ya madini yaliyopo ili kufanya uchimbaji wenye tija,Mikopo na mitaji kwa wachimbaji wadogo,uongezaji wa thamani madini na masoko na utatuzi wa migogoro ya uchimbaji madini inayojitokeza.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari wa Mkoa wa Ruvuma

Agosti 2,2020

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.