Masoko ya madini ya vito na dhahabu ya Tunduru na Songea tangu kufunguliwa kwake Mei 2019 hadi kufikia Mei 2020 yamewezesha kununuliwa madini ya vito na dhahabu yenye uzito wa gramu 390,936.27 yenye thamani ya shilingi bilioni 5,534,894,572.49,mrabaha uliopatikana katika mauzo hayo ni shilingi milioni 332,093,674.35,ada ya ukaguzi iliyopatikana ni shilingi milioni 55,348,945.72 na kodi ya huduma iliyopatikana katika kipindi hicho ni shilingi milioni 16,604,683.72
Akitoa taarifa ya sekta ya madini mkoani Ruvuma katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi 2020, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme
Mkoa wa Ruvuma, katika juhudi za kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi imeendelea na utekelezaji wa shughuli mbalimbali kwa ajili ya kukuza Sekta ya Madini katika Mkoa. Kufuatia juhudi za Mhe. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sekta ya Madini Mkoa wa Ruvuma imekuwa kwa kasi katika maeneo ya uwekezaji kwenye leseni za uchimbaji, uzalishaji madini, ajira pamoja na makusanyo ya maduhuli ya Serikali. Jedwali lifuatalo linabainisha ongezeko katika maeneo hayo kwa ulinganisho kati ya mwaka 2015 na 2020.
Jedwali : Ongezeko la shughuli za uchimbaji na biashara ya madini pamoja na makusanyo ya maduhuli ya Serikali katika Sekta ya Madini – Mkoa wa Ruvuma
Na. |
KIPENGELE
|
Mwaka wa Fedha 2015/16 |
Mwaka wa Fedha 2019/20 |
Ongezeko (%) |
|
1 |
Kuongeza idadi ya Wamiliki wa Leseni za Uchimbaji
|
|
|
|
|
|
(i)
|
Leseni za uchimbaji Mdogo (PMLs)
|
283 |
1,171 |
313.78 |
|
(ii)
|
Leseni za uchimbaji wa Kati (MLs)
|
5 |
9 |
80.00 |
|
(iii)
|
Leseni za uchimbaji Mkubwa (SMLs)
|
1 |
1 |
- |
|
(iv)
|
Leseni za Utafiti wa Madini (PLs)
|
31 |
66 |
112.90 |
|
(v)
|
Leseni za Biashara Kubwa ya Madini (Dealers)
|
25 |
53 |
112.00 |
|
(v)
|
Leseni za Biashara ya Udalali wa Madini (Brokers)
|
12 |
60 |
400.00 |
|
(vi)
|
Viwanda vya Uchenjuaji wa Madini ya Dhahabu
|
- |
5 |
100.00 |
2 |
Kuongezeka kwa Makusanyo ya maduhuli serikalini (TZS)
|
1,034,131,469 |
7,465,795,848 |
621.94 |
|
3 |
Kuongezeka kwa uzalishaji na biashara ya makaa ya mawe (Tani)
|
248,243 |
636,758.76 |
156.51 |
|
4 |
Mauzo ya madini kwenye Masoko ya Madini ya dhahabu na Vito vya Thamani
|
|
|
|
|
|
(ii)
|
Thamani ya Mauzo ya Madini ya Dhahabu (TZS)
|
56,500,000 |
4,787,234,596 |
8,372.98 |
|
(ii)
|
Thamani ya Mauzo ya Vito vya Thamani (TZS)
|
500,300,000 |
1,304,763,172 |
160.80 |
Jedwali : Ongezeko la ajira katika Sekta ya Madini – Mkoa wa Ruvuma
Na |
|
AINA YA LESENI
|
IDADI YA AJIRA |
ONGEZEKO LA AJIRA KWA MWAKA DES 2015 – JUN 2020 |
||||
DES 2015 |
JUN 2020 |
|||||||
NDANI |
NJE |
NDANI |
NJE |
NDANI |
NJE |
|||
1 |
Leseni za uchimbaji Mkubwa (SMLs)
|
95 |
10 |
27 |
2 |
-68 |
-8 |
|
2 |
Leseni za uchimbaji wa Kati (MLs)
|
281 |
3 |
517 |
12 |
236 |
9 |
|
3 |
Leseni za uchimbaji Mdogo (PMLs)
|
20 |
0 |
102 |
0 |
82 |
0 |
|
4 |
Leseni za Bishara Kubwa ya Madini (Dealers)
|
30 |
15 |
102 |
35 |
72 |
20 |
|
5 |
Leseni za Bishara ya Udalali wa Madini (Brokers)
|
32 |
0 |
58 |
0 |
26 |
0 |
|
|
JUMLA
|
458 |
28 |
806 |
49 |
416 |
29 |
Katika kutatua changamoto wanazokabiliana nazo wachimbaji wadogo wa Madini nchini. Serikali inajenga kituo cha Umahiri kwa ajili ya wachimbaji wadogo.
Kituo hicho kina faida zifuatazo.
Upatikanaji wa maeneo; yaliyotengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo
Utoaji wa mafunzo na maarifa kwa Wachimbaji wadogo kupitia wadau mbalimbali;
Mfumo wa kutathmini mashapo ya madini yaliyopo ili kufanya uchimbaji wenye tija;
Mikopo na mitaji kwa wachimbaji wadogo;
Uongezaji wa thamani madini na masoko;
Utatuzi wa migogoro ya uchimbaji madini inayojitokeza.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.