Wakulima Wilayani Tunduru wameingiza Zaidi ya bilioni 9 baada ya kuuza Mbaazi tani 4,732 katika minada minne iliyofanyika kwa msimu huu wa mwaka 2023.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Mkuu TAMCU LTD ndg. Imani Kalembo, katika mnada wa nne uliofanyika katika kijiji cha Mkanyageni AMCOS ya Nakatete Wilayani Tunduru Septemba 14, 2023, amewahamasisha wakulima kuendelea kulima zao la Mbaazi kwa wingi kwa kuwa pamoja na kuwa ni zao la chakula lakini hivi karibuni limekua zao la biashara.
“Tunduru tuna bahati kubwa sana kwasababu tunalima mazao yanayofuatana kwa msimu, kwa hiyo mwaka mzima mkulima anakua ananufaika kwa kupata fedha kwa ajili ya maendeleo yake”. Alisema.
Aidha, katika Mnada wa nne kampuni 11 zilijitokeza kushiriki katika mnada huo, kampuni tatu zilifanikiwa kuingia katika ushindani ambapo zilifikia wastani wa bei ya kununua mbaazi kwa wakulima, ambapo tani 700 ziliuzwa kwa bei ya shilingi 2,015 kwa kilo moja.
Wakulima wameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mfumo wa Stakabadhi ghalani, ambao umeonekana kuwa na tija kwa mkulima.
Tulikua tunalima na kuuza mbaazi kwa bei ya chini sana kabla ya kuwepo mfumo wa stakabadhi ghalani, mfumo huu umekua ni mkombozi ukilinganisha na walanguzi waliokuwa wakinunua kwa bei ya kutupwa”. Hayo yalisemwa na Bi. Shakira Kazembe Bakari, Mkulima wa Mbaazi toka kijiji cha Mkanyageni.
Mnada huo ulihudhuriwa na wakulima wengi wa mbaazi huku wakionyesha furaha yao kwa bei ya juu iliyopatikana kwenye mnada huo ambayo iliongezeka ikilinganishwa na mnada wa tatu ambapo wakulima waliuza mbaazi kwa shilingi 1,948.Baadhi ya wakulima wa kijiji cha Mkanyageni wilayani Tunduru wakiwa kwenye mnada wa zao la mbaazi
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.