SERIKALI inatarajia kuanzisha Kanda Maalum ya kiuchumi {Special Economic Zone} katika eneo la Mbambabay ziwa Nyasa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma ili kuhakikisha bidhaa zote ambazo zinapatikana Kariakoo jijini Dar es salaam ziweze kupatikana Nyasa.
Hayo yamesema na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mheshimiwa Humphrey Polepole alipofanya ziara katika wilaya ya Nyasa kuangalia fursa za uwekezaji katika ushoroba wa Mtwara,unaonzia mkoani Mtwara hadi Mbambabay ziwa Nyasa.
Balozi Polepole ametoa rai kwa wadau wa maendeleo kuwa tayari kutumia fursa zote zinazopatikana katika ushoroba wa Mtwara.
“Ushoroba huu ni wa barabara inayotoka bandari ya Mtwara hadi Mbambabay kwa kilometa 822 mpaka bandari ya Mbambabay,ushoroba huu kusini mwa Afrika,ndiyo ushoroba bora zaidi na mfupi kuliko shoroba nyingine zote’’,alisema.
Amesema ushoroba wa Mtwara -Mbambabay umesheheni madini ya aina mbalimbali yakiwemo makaa ya m awe,dhahabu,uranium na madini mengine ambayo ni fursa kwa wakazi wa eneo lote la ushoroba.
Pole pole amesema wamedhamiria kuhakikisha ushoroba wa Mtwara -Mbambabay unatangazwa na kuwa mbadala wa ushoraba wa Dar es salaam kwa sababu Dar es salaam hadi Lilongwe ni Kilometa 1600 wakati Ushoroba wa Mtwara ni kilometa 900.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.