SHULE ya sekondari ya Mbinga Girls ambayo inamilikiwa na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma imeendelea kupata mafanikio makubwa kitaaluma tangu kuanzishwa kwake mwaka 2014.
Mkuu wa shule hiyo Efigenia Nzota amesema shule hiyo yenye kidato cha kwanza hadi cha nne ilianzishwa kwa ajili ya wanafunzi wa kike ambapo ilianza kutoa wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2017 kwa kufaulisha kwa asilimia 95 ambapo kati ya wahitimu 68 walifanya mtihani waliopata sifuri walikuwa watatu.
Nzota amesema mwaka 2018 jumla ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne walikuwa 77 ambapo shule hiyo iliweza kufaulisha kwa asilimia 98 na kwamba ni mwanafunzi mmoja tu ndiyo alipata daraja sifuri.
“Mwaka 2019 tulikuwa na watahiniwa 108 ufaulu wetu ulikuwa kwa asilimia 100,matokeo haya ndiyo yaliyotuwezesha kupata tuzo baada ya kuingia katika shule kumi bora kitaifa katika kundi la shule za wananchi kwa kushika nafasi ya sita kati ya kumi’’,alisema.
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa shule,Mbinga Girls imeendelea kupata mafanikio makubwa kitaaluma ambapo mwaka 2020,shule hiyo ilifaulisha kwa asilimia 100 kutokana na watahiniwa 93 kufanya mtihani na kufaulu wote.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.