Ukatili wa kingono umekuwa ukufanyika katika jamii ambapo kesi nyingi zimekuwa azilipotiwi kwa wakati. Makosa yanayo jitokeza Vijijini na Mijini kumekuwepo na dhana ya kuwa mtuhumiwa ni ndugu wakaribu, yaweza kuwa ni mwenye cheo au wadhifa fulani katika familia husika, ambapo kwa namnamoja au nyingine dhana hiyo imekuwa kama kinga kuwaficha wahalifu hao na kufanya ukatili huo kuendelea kuwepo kwakuwa watuhumiwa hawachukuliwi hatua za kisheria
Semina hiyo ilio kuwa ikitolewa na mashirika ya CSSC, PACT, PEPFAR,na USAID wakiwashirikisha viongozi katika ngazi ya kata wakiwemo Walimu,Watendaji wa kata, Wazee wa Mila, Wachungaji, Polisi Dawati la jinsia na Madiwani . Viongozi hao wametakiwa kuwa wafuatiliaji pamoja ya kwamba wao ni viongozi na pia ni wazazi wanapaswa kujua niwapi mtoto anaweza kuwepo na kwa usalama kiasi gani
Maeneo kama Nyumbani, Mashuleni na maeneo yanayo tuzunguka yamebainishwa kuwa na ukatili wa kingono kwa watoto, na kwamba viongozi hawo wametakiwa kushirikiana kuwabaini watuhumiwa, bila kujali nafasi au wadhifa wa mtu alionao ili kuwafikisha katika vyombo vya sheria. Pia viongozi hao wametakiwa kuwa wafuatiliaji wa kesi hizo na kuakikisha sheria ifuatwe pindi itathibitika kufanyika ukatili huo.
Ata hivyo utolewaji wa taarifa kwa matukio ya ukatili wa kingono imeshauriwa yawe yenye usiri katika jamii hii itasaidia vyombo vya usalama kufanya uchunguzi kwa usahii na kuwabaini watuhumiwa pasipo na shaka. Kama viongozi pia yatupasa kumwakikishia mtoto kua sioyeye mtenda kosa, kumwamini hii itampa mtoto ujasili kusaidia kupata taarifa sahii na mapema
Utambuzi wa lasilimali zinazo tuzunguka kama Vituo vya Afya, Wataalamu wa Sheria, Dawati la jinsia, Usalama wa polisi, kama viongozi watambue hilo na pia kiongozi anawajibu kuzikemea mila potofu kwa jamii ,tukiyafanya hayo kwa kushirikiana tutaweza kuepuka Ukatili wa Kingono kwa watoto na jamii kwa ujumla
Imetolewa na Kaimu Afisa Habari Mbinga, Christian Makangury
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.