WILAYA ya Mbinga mkoani Ruvuma ina upungufu wa watumishi wa afya 1,718 kati ya mahitaji ya watumishi 2,366 wanahitajika katika Divisheni ya Huduma ya Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mheshimiwa Aziza Mangosongo wakati anatoa taarifa ya Wilaya hiyo kwa Naibu Waziri wa Afya DR.Godwin Mollel ambaye amefanya ziara ya kikazi ya siku mbili Wilayani Mbinga.
Mangosongo amebainisha kuwa watumishi wa afya waliopo wilayani humo ni 648 na kwamba kati yao katika Halmashauri ya Mbinga mji wapo watumishi 319 na upungufu ni watumishi 864.
Amewataja watumishi wa afya waliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kuwa ni 329 na upungufu ni watumishi 854.
“Mheshimiwa Naibu Waziri kwa ujumla Wilaya ina upungufu mkubwa wa watumishi wa Divisheni ya Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii hivyo tunaiomba serikali kupitia Wizara ya afya mtukumbuke na kutuangalia kwa jicho la ziada tuna upungufu mkubwa wa watumishi “,alisisitiza Mangosongo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Mbinga amesema hadi kufikia Juni 2023 Wilaya hiyo imetumia zaidi ya shilingi bilioni 4.6 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya na nyumba za watumishi.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo Naibu Waziri wa Afya DR.Godwin Mollel ameipongeza Wilaya ya Mbinga kwa usimamiaji mzuri wa miradi ya maendeleo.
Hata hivyo ameahidi kuhakikisha changamoto walizozitaja zinapatiwa ufumbuzi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.