Halmashauri ya Mji wa Mbinga, mkoani Ruvuma imeshika nafasi ya 10 ya mashindano ya Afya na Usafi wa Mazingira kwa ngazi ya miji nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa mashindano hayo yanayoratibiwa na Wizara ya Afya, Halmashauri ya Mji wa Mbinga kwa mwaka 2023 ilishika nafasi ya tisa kati ya Halmashauri za miji 21 zilizoshindanishwa nchini.
Katika nafasi hiyo, Mbinga Mji ilifungana na Halmashauri za miji ya Mbulu, Mkoa wa Manyara na Nanyamba,Mkoa wa Mtwara baada ya kupata asilimia 62 ya alama zote.
Halmshauri za miji zilizoitangulia Halmashauri ya Mbinga Mji ni Pamoja na Halmashauri za miji ya, Njombe asilimia kwenye mabano (89), Babati (73), Makambako (72), Nzega (71), Kibaha (70), Masasi (67), Mafinga (66) na Tunduma (64).
Halmashauri za miji zilizozidiwa na Halmashauri ya Mji Mbinga na asilimia zake kwenye mabano Halmashauri za miji Kasulu (56), Geita (56), Newala (56), Handeni (52), Ifakara (52), Tarime (46), Korogwe (46), Bunda (45), Bariadi (44) na Kondoa (30).
Akizungumza ofisini,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi. Amina Seif amewapongeza wakazi wa Mbinga Mji na wadau wengine kwa jitihada zao za kulivaa jukumu la usafi wa mazingira yao.
Afisa Afya wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bw. Felix Matembo amesema mafanikio waliyoyapata ni chachu kwa Mbinga Mji kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya mwaka 2024.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.