Mkuu wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mheshimiwa Aziza Mangosongo ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza makusanyo.
Mangosongo ametoa agizo hilo wakati anazungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga.
“Mbuni yanzo vipya vya mapato na vilivyopo mvilinde na kuvisimamia vizuri ili kuongeza mapato ya ndani,”alisisitiza Aziza.
Mkuu wa Wilaya ametaja Mapato kuwa ni ndiyo roho ya Halmashauri kwa kuwa bila mapato Halmashauri haiwezi kutekeleza shughuli za maendeleo kikamilifu.
Mangosongo amekemea tabia ya baadhi ya watumishi kutumia pesa mbichi kabla ya kuipeleka benki ambapo amesema tabia hiyo haikubaliki.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Amina Self amesema katika mwaka wa Fedha wa 2022/2023 Halmashauri ya Mji wa Mbinga ilikusanya Shilingi bilioni 2.128 kama mapato ya ndani.
Amesema katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 Halmashauri inatarajia kukusanya Shilingi bilioni 2.476 kama mapato ya ndani.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mheshimiwa Kelvin Mapunda amesema wamedhamiria kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa kuongeza kasi ya ukusanyaji ili kufikia na kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.