• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MBINGA yatoa hatimiliki za kimila zaidi ya 26,000 kwa vijiji 86,RC Ruvuma azindua

Imewekwa kuanzia tarehe: October 10th, 2020

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amezindua mpango wa kugawa hati miliki za kimila zaidi ya 1000  katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.

Mndeme  amezindua hati hizo kati ya hatimiliki zaidi ya 26,000 zilizotengenezwa na Halmashauri hiyo kwa ajili ya kugawawiwa vijiji 86  katika soko la Mnadani  kijiji cha   Nyoni.

,Mndeme amesema  Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ametimiza ahadi aliyotoa kwa  watanzania ya kuhakikisha migogoro ya ardhi inamalizika kwa kupanga kupima na kumilikisha kila kipande cha ardhi kwa kila mwananchi.

Mndeme amevitaja vijiji vitano vya Kata ya Nyoni ni kati ya vijiji 86  ambavyo vimenufaika na mpango wa hati miliki za kimila  katika Halmashauri ya wilaya ya Mbinga . Katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amewakabidhi hati  wakulima 20 wa Kata ya Nyoni   kwa niaba ya kata 24 zilizopo ndani ya Halmashauri  ya Wilaya ya Mbinga.

“Naomba Kuanzia sasa watu wa Benki  mzitambue   nyaraka hizi za hati miliki za kimila kuwa ni halali na wanaweza kuzitumia sehemu yeyote na vyombo vya kisheria kwa sababu mashamba haya yanakwenda kutambulika rasimi”. Amesema Mndeme.Mndeme pia amewapongeza Mkuu wa Wilaya ya Mbinga na Mkurugenzi wa Halmashauri kwa kufanikisha zoezi hilo  ambalo limegharimu zaidi ya shilingi bilioni moja katika  upimaji wa mashamba ambao umehusisha vijiji 86 vyenye ekari takiribani 59,000.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Cosmas Nshenye amesema atahakikisha kila kipande ambacho kipo katika halmashauri ya  Wilaya ya Mbinga kinapimwa  ambapo ametoa rai kwa wananchi  ambao hawajapimiwa kuondoa hofu kuhusu zoezi hilo ambalo ni endelevu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbinga Juma Mnwele, amesema ekari 70,000 ya mashamba ya mazao ya kudumu ambayo ni  sawa na mashamba 26,247 yametambuliwa na kupimwa.Hata hivyo Mnwele amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imeweza kutengeneza hatimiliki za kimila 26,247 katika vijiji 86  zilizogharimu zaidi ya shilingi bilioni moja  na vijiji hivyo ni  kati ya  vijiji 117 vya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.

Naye mkulima  wa kijiji cha  Nyoni  Ponziana Nzuyu amemshukuru Rais Dkt.John Magufuli  kwa kuwaunga mkono wakulima ambapo ametoa rai kwa wataalam kuendelea kuwaelimisha wananchi faida za hatimiliki.

Imeandaliwa na Farida Mussa 

Kutoka Ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma

Oktoba 10,2029

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.