SERIKALI Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 2.24 kutokana na fedha za asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Fedha hizo zimetolewa na Halmashauri za Mbinga Mji na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 hadi 2022/23 ambapo wanawake ndiyo walionufaika zaidi ya fedha hizo.
Hayo yalibainishwa wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Wilaya ya Mbinga katika kata ya Kitula ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Pascar Ndunguru alisema kati ya Shilingi bilioni 2.24, Shilingi bilioni 1.51 zilikwenda Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na Shilingi milioni 731.58 Halmashauri ya Mji wa Mbinga.
Amesema kuwa mikopo hii imetoa fursa za mitaji na uwekezaji kwa vikundi 371 Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na vikundi 197 Halmashauri ya Mji wa Mbinga.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya aliwataka wanawake kuwa na nidhamu ya matumizi ya pesa.
“Mtaji ndio nguzo yako. Hata iweje usile msingi wako,tnataka mwanamke aweze kujisimamia mwenyewe na kujikomboa kiuchumi” alisema Mhe. Aziza.
Alisema lengo la Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ni kuwapa ujasiri wanawake katika kujikomboa kiuchumi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.