MBUNGE wa Jimbo la Namtumbo mkoani Ruvuma Mheshimiwa Vita Kawawa ameutumia ukumbi wa bwalo la chakula katika sekondari ya wasichana ya Mkoa wa Ruvuma ya Dkt.Samia Suluhu Hassan iliyojengwa eneo la Migelegele wilayani Namtumbo.
Mbunge ameutumia ukumbi huo kugawa majiko ya gesi 300 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 25 ambayo ameyatoa kwa wajasirimali wadogo ili kuhakikisha wajasirimali hao wanatumia nishati safi kupikia.
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan hadi sasa imetoa shilingi bilioni 4.45 kujenga sekondari hiyo ambayo hadi sasa ina wanafunzi 600 wanaosoma katika sekondari hiyo yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 1000 wanaosoma kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.