MBUNGE KAWAWA AAINISHA MAFANIKIO YA MAENDELEO LIGERA NAMTUMBO
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo mkoani Ruvuma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Vita Kawawa, ametaja miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake Akihutubia wananchi wa Kata ya Ligera, alisema serikali imewekeza mabilioni ya shilingi katika sekta za afya, elimu, na miundombinu kwa manufaa ya wakazi wa Kata ya Ligera na Wilaya ya Namtumbo kwa ujumla.
Katika sekta ya afya, Kawawa alibainisha kuwa serikali imejenga Kituo cha Afya katika Kata ya Ligera kwa gharama ya shilingi milioni 500 na kukipatia vifaa tiba. Alisema juhudi hizo ni sehemu ya mpango wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wa kuboresha huduma za afya kwa makundi mbalimbali ya wananchi.
Kuhusu sekta ya elimu , Mbunge huyo alieleza kuwa shule mpya ya msingi imejengwa katika Kijiji cha Mtelawamwahi kwa gharama ya shilingi milioni 360,
Amesema Shule ya msingi Ligera ilipata madarasa mawili na vyoo kwa shilingi milioni 59, huku shule ya Njomlole ikipokea milioni 46 kwa madarasa mawili na milioni minne kwa ukarabati.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.