Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya amekabidhi chakula kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika Kata ya Lituhi wilayani Nyasa
Makabidhiano yamefanywa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa shanel Mbunda, katika viwanja vya Ofisi ya Afisa Mtendaji Kijiji Cha Kihuru Kata ya Lituhi.
Akikabidhi chakula hicho kwa waathirika wa mafuriko, amesema ametumwa na Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya kuwapa pole na kuwakabidhi chakula, baada ya mafuriko kubomoa nyumba za wakazi wa Lituhi, na baadhi ya mashamba kuharibika.
Msaada uliotolewa na Mbunge huyo ni mchele kilo 500 ambao umetolewa kwa waathirika 45 katika kaya 12.
Wakipokea chakula, wananchi wa Kata ya Lituhi wamemshukuru na kumpongeza Mbunge kwa Kwa msaada aliyoutoa.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Lituhi amesema wananchi wamefarijika sana baada ya kupewa chakula hicho kwa kuwa walikuwa na uhitaji baada ya kutokea mafuriko hayo.
Mafuriko yametokea hivi karibuni katika Kata ya Lituhi baada ya maji kupita katika makazi ya watu na kuharibu, mashamba,Nyumba na miundombinu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.