Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya amewataka wenyeviti wa vijiji,vitongoji na mitaa kuhakikisha wanashirikiana na wananchi kusimamia miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Manyanya ameyasema hayo wakati akizungumza na wenyeviti hao katika Ukumbi wa ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Nyasa kwenye Ukumbi wa shule ya Sekondari Tingi.
Amefafanua kuwa Viongozi hao wanatakiwa kuwashirikisha Wananchi kushiriki kikamilifu katika maendeleo yao, na kwamba maendeleo yanaanza na sehemu ya kutolea maamuzi ambayo ni Ofisi za vijiji na Vitongoji,.
Ametoa wito Kwa Viongozi hao kuanza Mara Moja mikakati ya ujenzi wa Ofisi za vijiji.pia amewapongeza Kwa kuchaguliwa Kwao na kuwataka kuchapa kazi Kwa bidii Kwa kuwa Wananchi wanahitaji maendeleo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.