Katibu Mkuu wa chama cha Mchezo wa Baseball na Softball Association Tanzania Alpherio Nchimbi amekabidhi vifaa vya mchezo huo kwa Kaimu afisa Michezo wa Mkoa wa Ruvuma Anzawe Chaula.
Makabidhiano hayo ya vifaa vya michezo ya wanafunzi wa shule za sekondari yalifanyika jana katika ofisi ya sekisheni ya Elimu Mkoa wa Ruvuma.
Nchimbi amesema vifaa vilivyotolewa ni kwa ajili ya kujikita katika mashindano ya UMISETA ikifuatiwa na agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa mgeni rasmi wakati anafungua uwanja wa Taifa wa baseball katika uwanja wa Azania sekondari Dar es salaam Desemba 2018.
“Chama cha michezo cha Baseball ni chama cha kwanza kumiliki uwanja wake juhudi hizo zimesababisha Serikali ya Japan kuamua kutufadhili”.alisema Nchimbi
Amesema Kwa Mikoani mchezo huo unachezwa katika viwanja vya kawaida ambavyo wataalamu wameweka vipimo katika viwanja hivyo.
Hata hivyo amesema Kutokana na Juhudi za mkoa wa Ruvuma watashauriana na kamati kuu kumpata mchezaji mmoja wa kuwakilisha mchezo wa softball kwenda kuwakilisha nchi ya Tanzania 2021
Nchimbi amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi sita Duniani zilizobahatika kupata nafasi ya kupeleka timu kabla ya olimpic ya mwaka 2020 na kuhairishwa hadi mwaka 2021 kutokana na ugonjwa wa Corona.
Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma Anzawe Chaula amesema Mkoa wa Ruvuma ni mkoa wenye vipaji vingi lakini macho ya wengi yanaangalia kwenye soka tu hali iliyosababisha hadi kuhangaika na timu ya Majimaji kuipandisha daraja.
Chaula amesma mkoa wa Ruvuma ni mkoa wanne nchini kuwa chama cha mchezo wa baseball na softball ambacho kimesajiliwa na ni kitu kipya hivyo amesahauri uwekezaji mzuri kufanyika kwa kuwa mchezaji mmoja kutoka Ruvuma anawakilisha Nchi ya Tanzania.
Imeendaliwa na Aneth Ndonde
Ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Tarehe 25 Agosti
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.