Serikali ya Awamu ya kwanza ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoongozwa na Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere kama zilivyoserikali zilizofuatia ilinunua meli mbli za kubebba abiria katika ziwa Nyasa ambapo meli za Mv.Songea ,MV. Iringa na MV Mbeya I zilinunuliwa na kutoa huduma kwa wananchi wa mikoa ya Mbeya,Njombe na Ruvuma.
MV Songea ni meli ya abiria na mizigo inayofanya safari katika Ziwa Nyasa. Ilikuwa inatoa huduma ya usafiri wa kibiashara na kwa abiria. Meli hii ilisaidia sana katika kuunganisha miji na vijiji vilivyo mwambao mwa ziwa Nyasa kwenye mikoa ya Mbeya,Njombe na Ruvuma
MV Iringa ni meli nyingine ya abiria na mizigo iliyokuwa inafanya kazi katika Ziwa Nyasa. Kama MV Songea, MV Iringa ilitumika katika kutoa huduma za usafiri kwa watu na bidhaa kwenye ziwa hilo. Meli kwa muda mrefu zilikuwa njia muhimu ya mawasiliano na biashara katika sehemu hii ya kusini mwa Tanzania.
Ziwa Nyasa linatumiwa kwa usafiri wa majini kwa sababu ya ukubwa wake na umuhimu wake kiuchumi. Meli kama MV Songea na MV Iringa zilichangia katika maendeleo ya eneo hili kwa kurahisisha usafiri na kubadilishana bidhaa na huduma.
Meli ya MV Iringa wakati huo ikiwa imetia nanga katika bandari ya Liuli wilayani Nyasa mkoani Ruvuma
Hata hivyo serikali za awamu ya Tano na Sita zimeendelea kuboresha usafiri wa majini katika ziwa Nyasa baada ya kununua Meli za MV Mbeya II, MV Ruvuma, na MV Njombe ni meli zinazofanya kazi katika Ziwa Nyasa na zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.