Menejimenti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki imekagua miradi minne ya afya katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga yenye thamani ya shilingi milioni 900.
Miradi iliyokaguliwa ni ujenzi wa kituo cha afya Mbangamao wenye thamani ya shilingi milioni 500,kituo cha afya Miyangayanga chenye thamani ya shilingi milioni 250,mradi wa nyumba ya mtumishi ya familia tatu katika kituo cha afya Kalembo iliyogharimu shilingi milioni 90 na zahanati ya Kijiji cha Matarawe iliyogharimu shilingi milioni 67.
Akizungumza baada ya kukagua miradi hiyo Ndaki ameipongeza Halmashauri ya Mji wa Mbinga kwa kusimamia miradi hiyo,hata hivyo ameagiza dosari zilizojitokeza katika hatua za umaliziaji hasa kwenye milango zifanyiwe marekebisho.Katibu Tawala huyo ameagiza kasi ya kukamilisha miradi kwa wakati na kwamba miradi yote ikamilike kwa asilimia 100 ili ianze kutoa huduma kwa wananchi.
Mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Mbangamao Halmashauri ya Mji wa Mbinga ambapo serikali imetoa shilingi milioni 500 kutekeleza mradi huo
Mradi wa ujenzi wa nyumba ya mtumishi yenye uwezo wa kuchukua familia tatu katika kituo cha afya Kalembo Halmashauri ya Mji wa Mbinga ambayo serikali imetoa shilingi milioni 90 kutekeleza mradi huo ambao tayari umekamilika
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.