MENEJIMENTI Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki imekagua mradi wa ujenzi wa sekondari mpya Kata ya Lusonga Halmashauri ya Mji Mbinga ambayo serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ilitoa shilingi milioni 470 kutekeleza mradi huo ambao tayari shule imesajiriwa na wanafunzi wameanza masomo.
Menejimenti hiyo imesema imetembelea shule mbalimbali katika Mkoa wa Ruvuma zinazotekeleza mradi wa programu ya uboreshaji elimu ya sekondari SEQUIP, ambapo Halmashauri ya mji wa Mbinga imetekeleza mradi huo kwa ufanisi mkubwa ukilinganisha na Halmashauri nyingine hivyo wanastahili pongezi.
Katika Mkoa wa Ruvuma kupitia programu ya SEQUIP serikali imetoa shilingi bilioni 7.7 kujenga sekondari mpya 11
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.