WALIMU wa Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma wapewa mafunzo ya uanzishwaji wa vitalu na upandaji Miti Mashuleni katika Shule shule nne za msingi
Mafunzo hayo yametolewa na Mtendaji Mkuu Mfuko wa Misitu Tanzania Taasisi ambayo ipo chini ya Wizara ya maliasili na Utalii Tuli Msuya katika ukumbi wa Halmashauri kwa shule za Msingi nne Njege,Lilondo,Mahanje,na Igawisenga.
Amesema kupitia mradi huo wadau lazima wawe wameanza kutekeleza mradi wa uhifadhi ili wapatiwe ruzuku kwaajili ya uwezeshaji wa mradi ambao ulioanza kutekelezwa.
Msuya amesema mradi huo ni chanzo cha uhakika na niendelevu kwaajili ya kugharamia ,kuwezesha na uhifadhi wa maliasili na misitu Nchini Tanzania ikiwa mfuko huo unatoa uwezeshaji kupitia ruzuku kwa wadau ambao wanawasilisha maombi kwaajili ya kuomba ruzuku dirisha la maombi hutolewa Desemba na kufungwa Machi kila Mwaka.
Msuya amesema ruzuku hiyo inatolewa kwa Mikoa yote Tanzania Bara ikiwa kwa Mkoa wa Ruvuma wameanza na Wilaya tatu Songea,Mbinga na Nyasa.
“Nawasihi sana Walimu pamoja na viongozi wa Halmashauri mhamasishe Shule wawasilishe maandiko kwaajili ya kunufaika na mradi”.
Amesema Ruzuku hiyo hutolewa kwa watu wote kwa maana watu binafsi,vikundi vya kijamii,asasi za kiraia, Taasisi za Serikali,Taasisi za kidini, Watafiti na mashirika yasiyo ya kiserikari.
Msuya ametaja lengo la mradi huo wa uanzishwaji wa vitalu na upandaji miti ni kwaajili ya kuiweka Tanzania kuwa kijani na watanzania kuendelea kupata hewa ya oksijeni, hivyo shule ambazo zimepatiwa mafunzo na kupewa ruzuku wataotesha vitalu na kugawa miche katika Shule zingine pamoja na wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.