Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa mafunzo ya mfumo wa M-MMA kwa Maafisa Habari na Watoa Elimu ya Afya kwa Umma ngazi ya Halmashauri ili kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na Wajawazito na Watoto Wachanga katika jamii.
Akizungumza wakati kufunga mafunzo hayo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr. lious Chomboko amewataka Washiriki kwenda kuyafanyia kazi kwa umakini mafunzo hayo kwa lengo la kutimiza adhima ya Serikali ya kuokoa maisha ya Wajawazito na Watoto Wachanga.
Chomboko amesema lengo la serikali ni kuona idadi ya vifo vya Wajawazito na Watoto Wachanga katika jamini hivyo waende kusimamia na kutoa elimu zaidi katika jamii kutumia elimu waliyopata katika mafunzo hayo.
“Serikali ikishirikiana na wadau imeamua kuongeza nguvu ya kupunguza idadi ya vifo hivyo kupitia Mfumo huu wa M-MMA ambao unahusisha Usafirishaji wa Dharura kwa Wajawazito na Watoto Wachanga lengo ni kunusuru maisha ya wajawazito na watoto kutumia huduma ambapo sasa unashushwa hadi ngazi ya jami ” amesema Dr chomboko
Naye Mratibu wa mwezeshaji wa mfumo wa Usafirishaji wa Dharura kwa Wajawazito na Watoto Wachanga (M-MMA) kitaifa, Hamady Rashidi Ally amesema mafunzo hayo ni kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuelimisha matumizi ya namba ya huduma ya 115 ambayo utimika kwa Dharura pindi inapoitajika msahada kwa Wajawazito na Watoto Wachanga.
Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo Mratibu wa mfumo wa M-MMA Mkoa wa Ruvuma Frida Meta amesema wanaishukuru serikali kwa kuwawezesha mafunzo hayo kwani yanaenda kupunguza idadi ya vifo vile vile jamii itapata elimu kuhusu matumizi sahihi ya namba ya msahada 115
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.