Picha juu ni Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati anazindua soko jipya la madini ya dhahabu na vito wilayani Tunduru
Uzalishaji wa madini ya makaa ya mawe katika Mkoa wa Ruvuma umeendelea kuwa chanzo muhimu cha mapato ya serikali katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Katika mwaka wa fedha 2023/2024, serikali iliuza tani 1,356,249.84 za makaa ya mawe zenye thamani ya zaidi ya Dola milioni 144.9 za Marekani.
Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Alphonce Bikulamchi, amesema kupitia mauzo hayo, serikali ilikusanya mrabaha wa Dola 3,937,434.98 na ada ya ukaguzi ya Dola 914,034.68. Madini hayo yameuzwa ndani ya nchi na kusafirishwa katika nchi jirani, barani Ulaya na Asia kupitia bandari za Mtwara na Dar es Salaam.
“Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Ruvuma imeendelea kutoa leseni za uchimbaji na biashara ya madini, ikiwemo leseni za uchimbaji mdogo (PML) na leseni za madini ya biashara kwa madalali (Dealers na Brokers), idadi ya leseni zilizotolewa imekuwa ikiongezeka, ambapo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2024/2025, mkoa una jumla ya leseni 144 za utafutaji madini na uchimbaji mkubwa na wa kati’’,alisema Mhandisi Bikulamchi,
Kwa mujibu wa Bikulamchi,Katika ukusanyaji wa maduhuli, Ofisi ya Madini Mkoa wa Ruvuma ilikusanya jumla ya shilingi 105,120,541,415.03 kati ya mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2024/2025, sawa na asilimia 126 ya lengo la makusanyo.
Mhandisi Bikulamchi anasema ongezeko la makusanyo haya ni ishara ya usimamizi mzuri wa sekta ya madini na kuimarika kwa mauzo ya madini hayo.
Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa michache nchini iliyobarikiwa kuwa na utajiri wa madini ya aina mbalimbali
Picha chini ni Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa alipotembelea Mgodi wa makaa ya mawe wa JITEGEMEE wilayani Mbinga
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.