Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imeanza kutekeleza ujenzi wa bandari mpya ya kisasa ya Mbambabay ziwa Nyasa wilayani Nyasa mkoani Ruvuma kwa gharama ya shilingi bilioni 70 lengo likiwa ni kuimarisha ushoroba wa maendeleo ya Mtwara ambayo ni njia fupi na rahisi kuhudumia mizigo ya Malawi kutokea bandari ya Mtwara.
Mradi huo unatarajia kukamilika ndani ya miezi 24,ujenzi wa bandari ya Mbambabay ukikamilika utaongeza uwezo wa kuhudumia shehena ya mizigo katika bandari kutoka tani 110,000 hadi kufikia tani 550,000 kwa mwaka na kwamba baada ya ujenzi wa bandari mpya ya Mbambabay kukamilika,makao makuu ya bandari za ziwa Nyasa yatahamia Mbambabay wilayani Nyasa mkoani Ruvuma kutoka bandari ya Kiwira iliyopo wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na serikali katika bandari za ziwa Nyasa,katika kipindi cha miezi sita ya mwaka 2023/2024 bandari zimehudumia jumla ya abiria 7,358 na mizigo tani 1,828.6.Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inasimamia bandari 15 katika ziwa Nyasa zilizopo katika mikoa ya Ruvuma,Mbeya na Njombe.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.