Wakulima wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wanataarifiwa kuwa miche bora ya korosho kwa msimu wa 2024/2025, awamu ya pili, inapatikana katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (Bomani) mjini Tunduru
Mratibu wa zao la korosho wilayani humo, Bwana Mussa Andendekisye Kibona, amesema miche hiyo imezalishwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Kituo cha Naliendele kwa kushirikiana na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT).
Miche hiyo inatolewa bure kwa wakulima waliokwishaandaa mashamba yao. Wanaohitaji wanapaswa kuwasiliana na maafisa kilimo wa kata kwa ajili ya taratibu za uchukuaji.
Bwana Kibona amewahimiza wakulima kutumia mvua zinazoendelea kunyesha ili kuhakikisha miche inapandwa kwa wakati, hali itakayochangia miche hiyo kuota na kustawi vizuri.
Serikali inalenga kuongeza eneo la kilimo cha korosho na kufanikisha uzalishaji wa tani 700,000 ifikapo msimu wa 2025/2026 na tani 1,000,000 ifikapo msimu wa 2029/2030.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.